Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (wa pili kushoto) akieleza majukumu ya Tume wakati wa mazungumzo baina ya Tume na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Canada nchini Tanzania yaliyofanyika Mei 25, 2023 Makao Makuu ya Ofisi za Tume, Kilimani jijini Dodoma.
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas akiongea na viongozi wa Tume (hawapo pichani) Mei 25, 2023 Makao Makuu ya Ofisi za Tume, Kilimani jijini Dodoma.
Mshauri wa masuala ya siasa, uchumi, na mambo ya umma kutoka Ubalozi wa Canada nchini, Bi. Sandra Rossister akiomba kuongea wakati wa mazungumzo baina ya Tume na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Canada yaliyofanyika Mei 25, 2023 Makao Makuu ya Ofisi za Tume, Kilimani jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Sheria Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bwana Nabor Assey akieleza kwa ufupi kuhusu utekelezaji wa tathimini ya masuala ya haki za binadamu nchini (UPR) wakati wa mazungumzo baina ya Tume na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Canada nchini Tanzania yaliyofanyika Mei 25, 2023 Makao Makuu ya Ofisi za Tume jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (katikati) na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Tume, Wahe. Dkt. Thomas Masanja (wa kwanza kulia) na Amina Talib Ali (wa pili kulia) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Mei 25, 2023 Makao Makuu ya Ofisi za Tume jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Maofisa Waandamizi kutoka Tume, Ofisi ya Ubalozi wa Canada nchini Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu akiagana na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Ofisi za Tume, Kilimani jijini Dodoma Mei 25, 2023.
BALOZI wa Canada nchini Tanzania, Mheshimiwa Kyle Nunas leo Mei 25, 2023 ametembelea Makao Makuu ya Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), jijini Dodoma na kufanya na mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujitambulisha kwa uongozi wa Tume, kujua masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa Tume na kujadiliana kuhusu maeneo mbalimbali ya mashirikiano katika kukuza na kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini.
Katika ziara yake hiyo Mhe. Balozi Nunas aliambatana na Mshauri wake wa masuala ya siasa, uchumi, na mambo ya umma, Bi. Sandra Rossister na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi.Salma Rajab Barak
Katika mazungumzo yao yaliyowashirikisha Makamishna na viongozi Waandamizi wa Tume, Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) pamoja na mambo mengine alielezea majukumu ya taasisi yake na namna Tume ilivyoshiriki katika uwasilishaji wa taarifa zake za tathimini ya hali ya haki za binadamu nchini (UPR) kwa mizunguko yote mitatu – 2011, 2016 na 2021, na namna inavyoshiriki katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa.
No comments:
Post a Comment