Wednesday, August 7, 2024

THBUB YATOA RIPOTI YA CHUNGUZI MBALIMBALI ILIZOFANYA KWA MWAKA 2023/24


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwasasa imeongeza kasi ya ushughulikiaji wa malalamiko ya uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kutokana na upatikanaji wa rasilimali fedha kwaajili ya uchunguzi ambapo kwa mwaka 2022/23 tume ilishughulikia jumla ya malalamiko 1524 ambapo ilihitimisha jumla ya malalamiko 789 na kufanya malalamiko yaliyoendelea orporate communications refers to the way in which businesses and organizations communicate with various internal and external audiences. These audiences commonly includ kuanzia Julai 1, 2023 kuwa 885.

Hayo yamebainishwa leo Julai 19,2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Mathew Mwaimu(Jaji Mstaafu) wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ripoti mbalimbali za chunguzi zilizofanywa na Tume kwa Mwaka wa 2023/24. “Aidha katika kioindi cha kuanzia Julai 10,2023 hadi Mei 30,2024 THBUB ilipokea malalamiko mapya 135 na kufanya malalamiko yanayoshughulikuwa mwaka huo kuwa malalamiko 1020 ambapo katika katika kipindi husika THBUB ilifanikiwa kukamilisha na kuhitimisha uchunguzi wa malalamiko 236 na hivyo uchunguzi wa malalamiko 784 unaendelea “,amesema.Mhe Mwaimu

Ameongeza kuwa katika malalamiko hayo, malalamiko 22 yaliilazimu THBUB kufanya uchunguzi maalum huku chunguzi hizo zikihusu masuala ya ardhi, uharibifu wa mazingira, tuhuma za vitendo vya ukatili katika vizuizi na matumizi mabaya ya madaraka. Sanjari na hayo Jaji Mstaafu Mwaimu amesema miongoni mwa chunguzi zilizofanyika ni tuhuma dhidi ya Jeshi la polisi ambapo tume ilithibitisha kutozingatiwa kwa taratibu za kisheria za ukamataji na ushikiliwaji wa watuhumiwa katika mahabusu ya polisi.

“Vitendo hivyo viliambatana na wananchi kupigwa, kufanyiwa ukatili na mateso na kusababishia majeraha mfano katika lalamiko la mwananchi kutoka Manispaa ya Morogoro, THBUB ilijiridhisha kuwa mwananchi huyo alipigwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili vilivyomsababishia majeraha akiwa anashikiliwa na askari wa jeshi la polisi mkoani Morogoro “,amesema.

Kuhusu chunguzi zilizohusu matumizi mabaya ya madaraka THBUB Jaji Mstaafu Mwaimu amesema ilifanya uchunguzi dhidi ya Mhe. Peuline Gekul kuhusu tukio la kuwaingiza chupa sehemu ya aja kubwa Bw. Hashim Ally na Bw. Michael Isaria na kubaini kuwa suala hilo halikufanyika.

“Hata hivyo THBUB ilibaini kuwa walalamikaji walizuiliwa kwa muda mrefu wakati wakihojiwa na mlalamikaji kuhusu tuhuma za kutaka kumwekea sumu Bi. Gekul pamoja na kupekelewa madawa ya kishirikina katika hotel yake na hivyo kusababisha walalamikajj kukosa haki yao ya kuwa huru”,amesema.

Aidha ameongeza kuwa uchunguzi mwingine ni kuhusiana malalamiko dhidi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda kuhusu kutoa amri ya kukamatwa na kuwekwa ndani ya mahabusu ya polisi mkazi mmoja wa Arusha na kubaini kuwa amri iliyotolewa haikuwa halali na haikuzingatia aina ya makosa. Amesema Tume itaendelea kufanya uchunguzi katika matukio yanayojitokeza na yenye viashiria vya uvunjifu wa amani nchini ili kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa mara moja katika jamii.


Tuesday, July 9, 2024

Tanzania kunufaika na Mradi wa”Sustainable Ocean Phase II"

Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazo nufaika na mradi wa “Sustainable Ocean Phase II"unaosimamiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Denmark(Danish Institute of Human Rights). Hayo yamebainishwa na Mshauri Mkuu wa Taasisi hiyo Bi.Carol Rask wakati walipotembelea Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hivi karibuni Jijini Dodoma. Bi.Carol alisema mradi huo unaotarajiwa kutaekelezwa kwa muda wa miaka minne unafadhiliwa na SIDA. “mradi huo umelenga kuimarisha ulinzi wa mazingira kwa wavuvi wadogo na jamii zinazowazunguka”alisema Bi.Carol Aidha Bi Carol alisema katika kutekeleza mradi huo wamefanya ziara nchini Tanzania iliyolenga kutafuta wadau mbalimbali ambapo moja ya wadau hao ni Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Bi Carol alisema wametembelea Tanzania ili kujifunza zaidi kuhusu maeneo yanayoweza kuzingatiwa ili kutekeleza mradi huo ikiwemo kukutana na Wadau mbalimbali ili kupata maoni yao pamoja na kuhakikisha watendaji wa Serikali na Sekta binafsi wanachukua hatua za kuimarisha haki za binadamu kwa wavuvi wadogo na jamii inayowazunguka kwa kuzingatia sheria za kitaifa,Sera na mipango inayohusiana na utawala wa wavuvi. Naye,Mratibu Miradi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi.Jovina Muchunguzi alisema kuwa Tume inaendelea na mchakato wa uwandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara kwa kushirikiana na wadau kutoka Serikalini na Sekta binafsi . "Tume imeshakutana na wadau hao na kuwaeleza hatua mbalimbali zilizofanyika za uandaaji wa mpango kazi huo"alisema Bi.Jovina Aidha ,Bi Jovina alisema kuwa Tume,katika mchakato wa uandaaji wa Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara eneo moja la kipaumbele ni kilimo na uchumi wa bluu ndani yake kuna shughuli za uvuvi. "Eneo hili ni muhimu katika maisha ya watanzania na katika mpango unaondaliwa"alisema Bi.Jovina Kwa hatua nyingine ujumbe huo ulieleza kuwa ipo tayari kushirikiana na Tume katika masuala ya Mafunzo,Tafiti,Kuandaa miongozo ya kusimamia haki za binadamu na masuala mengine. Ugeni huo ulipokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mohamed Khamis Hamad,Katibu Mtendaji Bwa.Patience Ntwina na baadaye mazungumzo hayo kuongozwa na Bi. Jovina Muchunguzi pamoja na Bw.Constatine Mugusi.

Tuesday, May 21, 2024

THBUB yaandaa Kikao Kazi cha Mapitio ya Maandiko, Machapisho na Nyaraka kuhusu Utekelezaji wa Biashara na Haki za Bindamu nchini.


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaendelea na hatua za Uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu utakaosaidia kuongeza uelewa wa wadau na jamii kuhusu ya Biashara na Haki za Binadamu na Mwongozo wa Kanuni za Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu kwa ujumla.

Hayo amebainisha Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Mohamed Khamisi Hamadi, wakati akifungua Kikao Kazi cha Mapitio (Literature Review) ya Mikataba ya Kimataifa, Kikanda, Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo, Maandiko na Machapisho mbalimbali yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu na biashara ili kutathmini utekelezaji wake na kuandaa taarifa hali ya utekelezaji, mapungufu, na kutoa mapendekezo yatakaosaidia kuchagua maeneo ya kipaumbele vitakavyoakisi mpango kazi huo.

Kikao kazi hicho kiliratibiwa na THBUB na miongoni mwa washiriki ni Waheshimiwa Makamishna wa THBUB, Katibu Mtendaji Msaidizi wa THBUB, Wakurugenzi kutoka THBUB, Watumishi wa THBUB, na Wadau kutoka Wizara za Kisekta, Idara na Taasisi za Serikali, pamoja na AZAKi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Kikao hicho kimefanyika tarehe 20 Mei, 2024 katika Ukumbi wa Golden Crest Jijini Arusha.

Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Mohamed alisema kuwa Kikao Kazi hicho kinaendelea kufanya mapitio ya Nyaraka, machapisho na maandiko mbalimbali kupitia makundi ya Kisekta “Thematic Working Groups” (TWGs) ambapo Timu ya Wataalamu imeandaa nyenzo za ukusanyaji wa taarifa hizo.

Mhe.Mohamed alitoa wito kwa washiriki kupitia vyema nyaraka hizo yanayohusu maeneo saba (7) ya vipaumbele vya kisekta vilivyoidhinishwa na Kamati Tendaji ya Kitaifa ambayo ni: Uziduaji na Nishati ,Uzalishaji na Usindikaji, Kilimo na Uchumi wa Buluu, Utalii na Ukarimu, Ujenzi na Usafirishaji, Mawasiliano ya Kidigital, na Biashara na Fedha.

"Kazi hii ya mapitio ya nyaraka ni muhimu sana kwaajili ya kuboresha Tathimin ya Hali ya Haki za Binadamu na Biashaara iliyofanywa na THBUB mwaka 2017" alisema Mhe. Mohamed. Aidha, Mhe. Mohamed alitoa shukrani kwa Serikali zote mbili, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Taasisi na Idara Serikali na Asasi za Kiraia kwa kuhakikisha THBUB inatekeleza vyema jukumu la kuratibu Uandaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadaku na Biashara.

THBUB ilifanya tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu na Biashara kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa Serikali kutoka pande zote za Muungano na Wadau wengine na kuendelea kushirikiana na wadau hao katika kueneza na kuhamasisha ajenda ya haki za binadamu na biashara nchini.


Friday, April 5, 2024

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB),Bwana Gabriel Robi akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa Watumishi wapya katika utumishi wa umma kutoka THBUB,Uongozi Institute,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mfuko wa Pembejeo, yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)jijini Dodoma, Aprili 3, 2024.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora anayeshughulika masuala ya Utawala, Bibi Portacia Benito akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo elekezi kwa Watumishi wapya katika utumishi wa umma kutoka THBUB,Uongozi Institute,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mfuko wa Pembejeo, yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa TBA jijini Dodoma, Aprili 3, 2024.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma,Bwana Maurice Nchimbi akitoa mada kuhusu Muundo wa Serikali na namna inavyoendesha shughuli zake wakati wa mafunzo elekezi kwa Watumishi wapya katika utumishi wa umma kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Uongozi Institute,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mfuko wa Pembejeo, yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa TBA jijini Dodoma, Aprili 3, 2024.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma,Bwana Charles Magaya akitoa mada kuhusu Utunzaji wa Kumbukumbu na Misingi ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma wakati wa mafunzo elekezi kwa Watumishi wapya katika utumishi wa umma kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Uongozi Institute,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mfuko wa Pembejeo, yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa TBA jijini Dodoma, Aprili 3, 2024.
Watumishi wapya kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Mfuko wa Pembejeo,Uongozi Institute na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,wakiwa katika mafunzo elekezi ukumbi wa mikutano wa TBA jijini Dodoma, Aprili 3, 2024.

Watumishi wa umma watakiwa kujua majukumu ya taasisi zao

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bwana Gabriel Robi amewataka watumishi wapya katika utumishi wa umma nchinikuyajua vyema majukumu ya taasisi zao na kutoa huduma bora kwa wananchi. Pia, amewataka watumishi hao kuwa na ushirikiano kazini, kutunza siri za ofisi, kuwa wavumilivu, na kuushirikisha uongozi pindi wapatapo changamoto mbalimbali. Bwana Robi ameyasema hayo leo Aprili 3, 2024 wakati akifungua mafunzo elekezi kwa watumishi wapya kutoka THBUB,Uongozi Institute,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mfuko wa Pembejeo (AGITF), yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) jijini Dodoma. “Baadhi ya watumishi wanayafahamu majukumu ya idara zao tu, lakini ufahamu wao ni mdogo juu ya majukumu ya taasisi;hili halikubaliki,” Kaimu Katibu Mtendaji huyo alisema, na kuongeza kuwa “ni wajibu wa kila mtumishi kujua majukumu ya taasisi yake.” Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi kutoka THBUB anayeshughulika masuala ya Utawala, Bibi Portacia Benito alimshukuru Bwana Robi kwa nasaha zake nzuri kwa watumishi wapya na kwa kufungua mafunzo hayo. Mafunzo hayo ya siku tatu yanaendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Dar es Salaam na yanatarajia kuongeza uwajibikaji mahala pa kazi, uzingatiwaji wa sheria, taratibu za kazi, na kuleta tija na ufanisi katika utendaji kazi. Jumla ya watumishi wapya 16, kati yao 10kutoka Ofisi kuu ya THBUBjijini Dodoma watanufaika na mafunzo hayo, ambapo mada mbalimbali, zikiwemo: Muundo wa Serikali na uendeshaji wake, Kanuni za utumishi wa umma, huduma bora kwa mteja na nyinginezo zitatolewa.

Saturday, March 30, 2024

THBUB yasaini makubaliano ya mashirikiano na MISA-TAN

Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bwana Patience Ntwina akitia saini hati ya makubaliano ya mashirikiano baina ya Tume na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN)Makao Makuu ya Tume Kilimani Jijini Dodoma leo Machi 28,2024.
Mkurugenzi Mtendaji waTaasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi.Elizabeth Riziki akitia sainihati ya makubaliano ya mashirikiano baina ya taasisi yake na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala BoraMakao Makuu ya Tume Kilimani Jijini Dodoma leo Machi 28,2024.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bwana Patience Ntwina na Mkurugenzi Mtendaji waMISA-TAN,Bi.Elizabeth Riziki wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) nakala za hati za makubaliano ya mashirikiano walizotia saini kwa niaba ya taasisi zao. Hafla ya utiaji saini hazi hizo imefanyika leo Machi 28,2024Makao Makuu ya Tume Kilimani Jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Khamis Hamad(katikati) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya MISA-TAN, Bwana James Marenga (wapilli kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Tume na viongozi waandamizi wa taasisi zao mara baada ya hafla fupi ya kutia saini hati ya makubalino ya mashirikiano leo Machi 28,2024Makao Makuu ya Tume Kilimani Jijini Dodoma. Wengine katika picha (waliokaa) ni: Mhe. Dkt. Thomas Masanja (wa pili kulia), Mhe. Amina Talib Ali (wa kwanza kulia), na Katibu Mtendaji wa MISA-TAN, Bi. Elizabeth Riziki (wa kwanza kushoto).

Friday, March 15, 2024

THBUB yatembelea hospitali ya Mirembe na kutoa msaada

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Amina Talib Ali (Kushoto) akimkabidhi Afisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Mirembe, Bi. Irene Kitula bidhaa mbalimbali zilizotolewa na Tume mara baada ya mazungumzo mafupi uongozi wa hospitali hiyo leo Machi 15, 2024.
Ujumbe wa watumishi wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiongozwa na Kamishna wa Tume, Mhe. Amina Talib wakizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dkt. Godwin Mwisombe ujumbe huo ulipotembelea taasisi hiyo leo Machi 15, 2024.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Amina Talib Ali akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili, Milembe iliyopo jijini Dodoma leo Machi 15, 2024.
Mkurugenzi Msaidizi - Utafiti na Nyaraka, Bi. Fides Shao akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili, Milembe jijini Dodoma leo Machi 15, 2024.


Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ujumbe wa watumishi wanawake kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) leo Machi 15, 2024 umetembelea Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe jijini Dodoma na kutoa msaada.

Akiongea wakati wa kukabidhi bidhaa mbalimbali Kiongozi wa ujumbe huo, Kamishna wa Tume, Mhe. Amina Talib Ali alisema kuwa lengo la ziara yao ni kuwafariji na kuwashika mkono wagonjwa wenye uhitaji maalum hosptalini hapo.

Aidha, Mhe. Amina, ambaye pia ni Msimamizi wa masuala ya makundi maalum katika THBUB alitoa pongezi kwa madaktari, wauguzi na watumishi wengine kwa kuwathamini na kujitoa kwao kuwahudumia wagonjwa waliopo hospitali hapo.

Mhe. Kamishna aliukabidhi uongozi wa hospitali ya Mirembe bidhaa zenye thamani ya jumla ya Shs. 610,000/=, zikijumuisha: sabuni za kufulia na kuogea, pampasi za watoto, mafuta ya kupaka, na maziwa. Bidhaa nyingine ni miswaki, dawa za meno, nguo za ndani, pamoja na unga wa lishe.

Akipokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt. Godwin Mwisombe aliishukuru THBUB kwa kuwakumbuka wahitaji waliopo hospitalini hapo. “Msaada huu ni wa muhimu sana na utasaidia kutatua baadhi ya changamoto zilizopo,” alisema.

Dkt. Mwisombe alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa umma kujiepusha na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ugonjwa wa akili na kuunga mkono jitihada za kuelimisha umma juu ya changamoto ya afya ya akili, ambayo inawakumba watu wengi kila uchao.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo watu wengi wana changamoto ya afya ya akili, na wachache ndiyo wenye ugonjwa wa akili, hivyo elimu inahitajika ili kulikinga kundi hilo kubwa lisipatwe na ugonjwa huo.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii hospitalini hapo, Bi. Irene Kitula alitoa wito kwa taasisi nyingine na watu binafsi kuiga mfano wa THBUB ili kuiwezesha hospitali hiyo kuwahudumia kikamilifu wagonjwa, ambapo baadhi yao wametekelezwa na familia zao.

Mwaka huu kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake yalifanyika kimkoa Machi 8 Viwanja vya Shule ya Chinangali wilayani Chamwino ambapo THBUB ilishiriki pia.