Sunday, January 21, 2024

THBUB Kushirikiana na Taasisi ya Haki za Binadamu Urusi

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Jaji mst. Mathew Mwaimu (katikati, kushoto) na viongozi wengine wa Tume wakiwa katika mazungumzo ya faragha na Wageni wao kabla ya kutiliana saini Makubaliano ya mashirikiano Ofisi Kuu ya Tume, Kilimani Jijini Dodoma leo Januari 20, 2024.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bwana Patience Ntwina akitia saini Makubaliano ya mashirikiano baina ya Tume na Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya nchini Urusi (Office of the High Commissioner for Human Rights in the Russian Federation) leo Januari 20, 2024 Ofisi Kuu ya Tume Kilimani, Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu akimkabidhi nyaraka mbalimbali za Tume Naibu Mkuu wa Utawala wa Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya nchini Urusi, Bwana Ilya Chechelnitskii mara baada ya kutiliana saina Makubaliano ya mashirikiano Ofisi Kuu ya Tume Kilimani, Jijini Dodoma leo Januari 20, 2024.
Mkuu wa masuala ya Habari waTaasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya nchini Urusi, Bi. Tatiana Dzhedzhula akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu Ofisi Kuu ya Tume Kilimani, Jijini Dodoma leo Januari 20, 2024.
Naibu Mkuu wa Utawala wa Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya nchini Urusi, Bwana Ilya Chechelnitskii akitoa zawadi kwa Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mst.) Ofisi Kuu ya Tume Kilimani, Jijini Dodoma leo Januari 20, 2024.


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ya Tanzania na Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya nchini Urusi (Office of the High Commissioner for Human Rights in the Russian Federation) leo Januari 20, 2024 zimetiliana saini makubaliano ya mashirikiano (MoU) katika kukuza na kulinda haki za binadamu katika mataifa yao.

Utilianaji saini makubaliano hayo umefanyika Ofisi Kuu ya THBUB Kilimani, Jijini Dodoma mbele ya vyombo vya habari, huku viongozi wa ngazi za juu wa taasisi hizo mbili wakishuhudia tukio hilo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji mst.) taasisi hizo zitashirikiana katika masuala ya mafunzo, kufanya tafiti, na kuandaa semina na makongamano ya kisayansi yanayolenga kuboresha mifumo ya shughuli za haki za binadamu katika ngazi za kitaifa na kikanda.

Pia, taasisi hizo zitafanya ziara na mikutano baina yao ili kubadilishana uzoefu, Mhe. Mwaimu alisema.

Katika hafla hiyo ya utilianaji saini makubaliano ya mashirikiano Mhe. Jaji Mstaafu Mwaimu aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Mohamed Khamis Hamad; Wahe. Makamishna wa Tume, Dkt. Thomas Masanja na Nyanda Shuli; na Katibu Mtendaji wa Tume, Bwana Patience Ntwina.

Wakati ujumbe wa Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya nchini Urusi uliongozwa na Naibu Mkuu wa Utawala, Bwana Ilya Chechelnitskii akiambatana na Mkuu wa Idara ya masuala ya Kimataifa, Bwana Viacheslav Tolmachev; Mtaalam wa masuala ya Kimataifa, Bwana Grigorii Malinkin; na Mkuu wa masuala ya Habari, Bi. Tatiana Dzhedzhula.

No comments:

Post a Comment