Watumishi Wanawake wa Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora tawi la Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuungana na Wanawake wenzao katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Mji Mwema wilayani Kigamboni, leo Machi 8, 2024.
Baadhi ya Watumishi Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ofisi Kuu Dodoma wakifuatilia hotuba wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali wilayani Chamwino leo Machi 8, 2024.

Baadhi ya Watumishi Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ofisi Kuu Dodoma wakiandamana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali wilayani Chamwino leo Machi 8, 2024.
Watumishi Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ofisi Kuu Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja huko Chamwino muda mfupi kabla ya kuanza kwa maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali wilayani Chamwino, leo Machi 8, 2024.

Watumishi Wanawake wa Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora tawi la Mwanza wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake yaliyofanyika kimkoa wilayani Misungwi, leo Machi 8, 2024. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Bi. Angela Mshana, alienda huko kikazi.
Baadhi ya Watumishi Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ofisi Kuu Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili huko Chamwino leo Machi 8, 2024. Aliyevaa ushungi na miwani (katikati) ni Kamishna wa THBUB, Mhe. Amina Talib Ali aliyewaongoza Wanawake hao katika maadhimisho hayo.
Kamishna wa THBUB na Msimamizi wa masuala ya Makundi Maalum, Mhe. Amina Talib Ali.
Leo Machi 8, 2024 Watumishi Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wameungana na wanawake wenzao nchini kote kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyobeba Kauli mbiu isemayo: “Wekeza kwa Wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii.”
Hakika ushiriki wao uliifanya siku hiyo kuwa ya kupendeza kutokana na mavazi mazuri na ya aina yake waliyoyavaa. Itoshe kusema, ‘pamba’ walizopiga zilivutia macho ya kila aliyewatazama – walipendeza!
Kamishna wa THBUB na Msimamizi wa masuala ya Makundi Maalum, Mhe. Amina Talib Ali aliwaongoza Wanawake hao katika maadhimisho hayo mkoani Dodoma, ambako kimkoa yalifanyika viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali wilayani Chamwino.
Uwepo wa THBUB pia ulionekana katika maadhimisho yaliyofanyika katika majiji ya Dar es Salaam na Mwanza ambako Tume inazo Ofisi zake za matawi.
Hii ni mara ya 27 Taifa letu linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyoridhiwa na Umoja wa Mataifa na kuanza kuadhimishwa kwingine duniani mwaka 1975.
No comments:
Post a Comment