Wednesday, June 23, 2021

WARSHA YA UWEZESHAJI SERIKALI NA WADAU WA HAKI ZA BINADAMU KUTIMIZA WAJIBU WAKE KATIKA KURIPOTIA ITIFAKI YA MKATABA WA AFRIKA KUHUSU HAKI ZA WANAWAKE

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (katikati) na Makamu wake, Mhe. Mohammed Khamis (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja washiriki wa warsha na wawezeshaji, Dodoma hotel jijini Dodoma Juni 22, 2021. Wa kwanza kushoto na wa kwanza kulia (waliokaa), ni Dkt. Ashwanee Budoo na Bi. Suzan Mutambasere, Wawezeshaji wa warsha kutoka Chuo Kikuu cha Pretoria cha Afrika Kusini. Wa pili kulia ni Kamishna wa Tume, Dkt. Fatma Khalfani.
Mshiriki kutoka TAWLA,Bi Penina Robert akichangia hoja wakati wa majadiliano
Baadhi ya washirika wa mafunzo wakifatilia mada.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),Bi.Anna Henga akichangia hoja wakati wa majadiliano.
Meneja wa Programu kuhusiana na haki za Wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Pretoria cha Afrika kusini Dkt.Ashwanee Budoo akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya uandishi wa ripoti za vitendo vya ukiukwaji wa haki za wanawake inayofanyika Dodoma hotel,jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kufungua warsha ya mafunzo ya uandishi wa ripoti za vitendo vya ukiukwaji wa haki za wanawake inayofanyika Dodoma hotel, jijini Dodoma.


Warsha hii ya siku tatu, iliyowahusisha washiriki takriban 35 kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Afya na Asasi za Kiraia imeandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na Kituo cha Haki za Binadamu cha Chuo Kikuu cha Pretoria cha Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment