Tuesday, June 29, 2021

THBUB YATOA MAFUNZO YA HAKI ZA BINADAMU KWA WATUMISHI WA AFYA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bwana Nabor Assey akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya hospitali ya rufaa Dodoma. Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo (Juni 25, 2021) katika ukumbi wa Bima ya Afya uliopo hospitalini hapo, na yamewahusisha takriban watumishi 30 wa kada mbalimbali
Afisa Uchunguzi Mkuu wa THBUB, Bwana Yohana Mcharo akiwasilisha mada katika warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma leo (Juni 25, 2021). Wengine katika picha ni watoa mada wenza kutoka THBUB, Bwana Peter Ntalika (wa kwanza kushoto) na Mwanyemi Bilali.
Sehemu ya Washiriki wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya hospitali ya rufaa Dodoma wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayuko pichani) leo (Juni 25, 2021).
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Mussa Shekimweri ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya hospitali ya rufaa Dodoma leo (Juni 25, 2021). Warsha hiyo ya siku moja imefanyika ukumbi wa Bima ya Afya ulipo hospitalini hapo
Kamishna wa THBUB. Mhe. Dkt. Fatma Khalfan akitoa neno katika warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya wa hospitali ya rufaa Dodoma muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi. Warsha hiyo imefanyika ukumbi wa Bima ya Afya hospitalini hapo leo (Juni 25, 2021).
Leo Juni 25, 2021, Jijini Dodoma: Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Mussa Shekimweri (katikati) na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Fatma Halfani (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma

No comments:

Post a Comment