Thursday, July 15, 2021

THBUB YAMUAGA BW. BARAKA BARAKA


Viongozi na Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) leo (Julai 14, 2021) wamemuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini, Bwana Baraka Baraka katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya taasisi hiyo eneo la Kilimani Jijini Dodoma.

Hivi karibuni Bwana Baraka aliteuliwa kuwa Mshauri wa Makamu wa Rais masuala ya Muungano.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Mohamed Hamis akitoa neno la shukran kwa niaba ya Tume katika hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango Tathmini na Ufuatiliaji Bwn. Baraka R. Baraka ambaye amehamia Ofisi ya Makamu wa Rais, hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi ya Tume Makao Makuu iliyopo Jijini Dodoma tarehe 14 Julai, 2021.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango Tathmini na Ufuatiliaji katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Bwn.Baraka R. Baraka akitoa neno la shukran kwa Tume katika hafla fupi ya kumuaga mtum
Afisa Uchunguzi Mwandamizi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora (THBUB) Kitengo cha Mipango Bwn. Mohamed Bakary akifungua Shampeni katika hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Kitengo hicho ambaye amehemia Ofisi ya Makamu wa Rais Bwn. Baraka R. Baraka iliyofanyika katika Ofisi ya Tume Makao Makuu Dodoma tarehe 14 Julai, 2021.
Bwn. Baraka R. Baraka (Kushoto) akimlisha Keki Kamishna waTume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Ofisi ya Zanzibar Mhe. Khatib Mwinyichande (Kulia) katika hafla fupi ya kumuaga Mtumishi huyo ambaye amehamia Ofisi ya Makamu wa Rais iliyofanyika tarehe 14 Julai, 2021.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora (THBUB) Mhe. Mohamed Hamis (Kulia) akiwa na Kamishna wa Tume hiyo kutoka Ofisi ya tawi la Dar es Salaam Mhe. Nyanda Shuli (Kushoto) katika hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mipango Bwn. Baraka R.Baraka ambaye amehamia Ofisi ya Makamu wa Rais iliyofanyika tarehe 14 Julai, 2021.
Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wakifuatilia matukio yaliyojiri katika hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mipango kwa Bwn. Baraka R. Baraka ambaye amehamia Ofisi ya Makamu wa Rais, hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi ya Tume Makao Makuu iliyopo Jijini Dodoma tarehe 14 Julai, 2021
Bwn. Baraka R. Baraka (Muagwa) akikata Keki katika hafla fupi ya kumuaga Mtumishi huyo iliyofanyika katika Ofisi ya Makao Makuu ya Tume iliyopo Jijini Dodoma tarehe 14 Julai,2021.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Mohamed Hamis (Kushoto) akimkabidhi zawadi kwa niaba ya Tume aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mipango Bwn. Baraka R. Baraka katika hafla fupi ya kumuaga Mtumishi huyo iliyofanyika katika Ofisi ya Makao Makuu ya Tume iliyopo Jijini Dodoma tarehe 14 Julai, 2021.
Kaimu Katibu Mtendaji waTume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Bwn.Nabor B. Assey (Kushoto) akiwa na Kamishna wa Tume hiyo kutoka Ofisi ya Tume Tawi la Dar es Salaam Mhe. Nyanda Shuli katika hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mipango Bwn. Baraka R. Baraka ambaye amehamia Ofisi ya Makamu wa Rais, hafla hiyo ilifanyika tarehe katika Ofisi ya Tume Makao Makuu iliyopo Jijini Dodoma tarehe 14 Julai, 2021.
Picha ya pamoja kàti ya Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) na aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mipango Bwn. Baraka R. Baraka (Watatu kutoka Kushoto) katika hafla fupi ya kumuaga Mtumishi huyo ambaye amehamia Ofisi ya Makamu wa Rais iliyofanyika katika Ofisi ya Tume Makao Makuu iliyopo Jijini Dodoma tarehe 14 Julai, 2021.

No comments:

Post a Comment