Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Mathew P.M Mwaimu (Jaji Mstahafu) akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu Maboresho na Mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki źa Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Mathew P.M Mwaimu-Jaji Mstahafu (kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Mohamed Hamis (Kushoto) wakifuatilia mada mbalimbali katika Warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu maboresho na mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021.
Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Tume ya Haki za bonadamu na Utawala Nora (THBUB) idara ya huduma za Kisheria Bwn. Constantine Mugusi ( Mshereheshaji) akisisitiza jambo katika Warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu maboresho na mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Bwn. Nabor B. Assey akitoa neno fupi kuhusu Tume na Mamlaka yake katika Warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu maboresho na mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021.
Jaji wa Mahakama Kuu na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Mahakama Mhe. Zahra Maruma akitoa Mada kuhusu Mpango Mkakati wa Mahakama na Mabadiliko katika Warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu maboresho na mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021.
Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wakifuatilia mada mbalimbali katika Warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu maboresho na mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021 Jijini Dodoma.
Wawezesha kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)kutoka Idara ya malalamiko na uchunguzi Bi. Jovina Muchunguzi (kulia) na Bwn. Yohana Mcharo (kushoto) wakiwasilisha Mada kuhusu aina ya malalamiko yanayopokelewa na Tume dhidi ya Mahakama ya Tanzania katika Warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu maboresho na mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021 Jijini Dodoma.
Afisa Uchunguzi Mkuu Msaidizi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Idara ya Malalamiko na Uchunguzi Bwn. Yohana Mcharo akiongea na chombo cha habari cha TBC1 katika Warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu maboresho na mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi ya Dar es Salaam Mhe. Nyanda Shuli akichangia mada katika Warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo kuhusu maboresho na mabadiliko katika uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mapema leo tarehe 13 Julai, 2021 Jijini Dodoma.
Mahakama Kuu ya Tanzania iliandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuhusu mabadiliko na maboresho katika uendeshaji wa shughuli za kimahakama nchini.
Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali tarehe 13 Julai, 2021 Jijini Dodoma.
Lengo la mafunzo haya ni kuongeza uelewa miongoni mwa watumishi wa Tume kuhsu maboresho na mabadiliko ya uendeshaji wa Mahakama nchini; kuimarisha na kuboresha mahusiano na mashirikiano yaliyopo baina ya Tune na Mahakama; Kujadili namna ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi;
Mafunzo haya yaliratibiwa na Mahakama ya Tanzania na yaliwasilishwa na wawakilishi kutoka Tume na Mahakama ya Tanzania. Wawasilishaji Mada walikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB Bwn. Nabor B. Assey (Tume na Mamlaka yake); Mhandisi Isack Manyiri- Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka THBUB (Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko Tume); Mhe. Zahra Maruma- Jaji wa Mahakama Kuu na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Mahakama (Mpango Mkakati wa Mahakama ba Mabadiliko); Ben. Allan D. Machela (Afisa TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania); Bwn.Khamadu Kitunzi; Mhe. Desidery Kamugisha - Mkurugenzi wa usimamizi wa malalamiko (Ushughulikiaji na usimamizi wa malalamiko katika Mahakama); Bi. Jovina Muchunguzi (Afisa Uchunguzi Mkuu Idara ya Malalamiko na Uchunguzi) na Bwn. Yohana Mcharo (Afisa Uchunguzi Mkuu Msaidizi Idara ya Malalamiko na Uchunguzi); Bi. Enziel Mtei - Naibu Katibu (Tume ya Mahakama).
Matarajio ya mafunzo haya ni kuongeza ufanisi baina ya taasisi hizi mbili katika kutekeleza majukumu hususan katika kushughulikia malalamiko ya wananchi kwani taasisi hizi mbili zinafanya kazi zinazofanana, kuboresha mashirikiano katika utendani kazi, kubadilishana uzoefu wa namna taasisi hizi mbili zinavyofanya kazi.
Taasisi zote hizi zimeahidi kuboresha mashirikiano na kufanya kazi kwa ukaribu zaidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa mustakabali wa nchi yetu.
Mafunzo haya yalifungwa na Makamu Mwenyekiti wa THBUB Mhe. Mohamed Hamis na aliahidi kwa niaba ya Tume kutekeleza yale waliyokubaliana.
No comments:
Post a Comment