Monday, January 23, 2023

THBUB YASHIRIKI UZINDUZI WA WIKI YA SHERIA

Mgeni Rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdor Mpango (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria uliofanyika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma Januari 22, 2023.
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakifuatilia kwa umakini hotuba wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma Januari 22, 2023.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bwana Patience Ntwina alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Taasisi mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Wiki ya Sheria jijini Dodoma. Uzinduzi huo uliambatana na matembezi ya kilometa 7 yaliyoanzia Kituo Jumuishi cha Haki (IJC).
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bwana Patience Ntwina (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Tume katika banda lao la maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza Januari 22, 2023 viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment