Wednesday, February 1, 2023

VIONGOZI WA TUME WASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA

Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Jaji Mst. Mathew Mwaimu (wa nne kushoto, waliosimama) na Majaji Wastaafu wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyofanyika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma Februari 1, 2023.
Baadhi ya Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, viwanja vya Chinangali jijini Dodoma Februari 1, 2023.
Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Jaji Mst. Mathew Mwaimu (wa pili kushoto) akiwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Othmani Chande (wa kwanza kushoto) pamoja na Majaji Wastaafu wengine wakiondoka katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma mara baada ya maadhimisho ya siku ya Sheria kukamilika Februari 1, 2023
Kamishna wa THBUB, Mhe. Nyanda Shuli (wa tatu kushoto) akifuatilia hotuba wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika Februari 1, 2023 viwanja vya Chinangali jijini. Wengine ni: Katibu Mtendaji wa Tume, Bwana Patience Ntwina (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bwana Nabor Assey (wa kwanza kushoto).

No comments:

Post a Comment