Saturday, February 11, 2023

NYANDUGA AAPISHWA KUWA KAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA





Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Awamu ya tatu, Mhe. Bahame Tom Nyanduga leo Februari 10, 2023 alikuwa miongoni mwa viongozi watatu walioapishwa kuwa Makamishna wapya wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Viongozi wengine waliokula kiapo hicho mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu, Chamwino jijini Dodoma ni Mhe. Jaji Ndika na Mhe. Dosca Mutabuzi.

No comments:

Post a Comment