Tuesday, May 2, 2023

Ushiriki wa THBUB katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2023

Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ofisi Kuu ya Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja viwanja vya Bunge jijini Dodoma kabla ya kuanza matembezi ya takriban kilometa 3 kuelekea uwanja wa Jamhuri Mei 1, 2023.
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ofisi Kuu ya Dodoma wakipita katika mitaa mbalimbali ya jijini Dodoma wakielekea uwanja wa Jamhuri yalikofanyika Maadhimisho ya Mei Mosi kimkoa. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (Mb) ndiye aliyeyapokea matembezi hayo kama Mgeni Rasmi.
Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ofisi Kuu ya Dodoma wakiwa na nyuso za furaha wakipita kwa kujiamini mbele ya jukwaa kuu uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Mei 1, 2023.
Viongozi wa juu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nao walijitokeza kwa wingi wao kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi, 2023 jijini Dodoma. Wakiwa jukwaa kuu, kutoka kulia ni: Makamishna wa Tume, Wahe. Dkt. Thomas Masanja na Amina Talib Ali na Katibu Mtendaji wa Tume, Bwana Patience Ntwina.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Khamis Hamad akiongea na vyombo vya habari wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Kitaifa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2023 yalifanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi.

Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ofisi ya Zanzibar na Ofisi za Matawi ya Dar es Salaam, Mwanza, Pemba na Lindi waliungana na wafanyakazi wengine katika kuadhimisha siku hiyo katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment